Wabaya wangu walitaka kuniua - Zuma

CAPE TOWN- RAIS Jacob Zuma amebainisha kwamba, wabaya wake
walijaribu kumuua kwa sumu kutokana na msimamo wake wa kufanya marekebisho ya
umiliki wa ardhi na kiuchumi.
Rais Zuma
aliyabainisha hayo Jumapili mwishoni mwa wiki iliyopita, alipokuwa akihutubia
mkutano wa chama chake cha African National Congress (ANC) mjini KwaZulu Natal.
“Niliwekewa
sumu ambayo ilikaribia kuniua, kwa sababu Afrika Kusini ilijiunga na Muungano
wa Brics unaounganisha mataifa ya Brazil, Urusi, India, China na jamii ya
kibiashara ya Afrika Kusini chini ya uongozi wangu.
“Walisema
nilikuwa nina mpango wa kuharibu nchi,” alisema Zuma.
Akihutubia
mkutano wa wanachama wa ANC huko Phongolo, Kwa Zulu Natal uliofanyika Jumapili,
Zuma alisema alilengwa alipotaka kuweka marekebisho makali ya kiuchumi.
Kulingana na
ripoti hiyo, kulikuwa na majaribio matatu ya kumuua. Hata hivyo, Zuma hakusema
ni nani aliyejaribu kumuua lakini anasema ni mtu wake wa karibu.
BBC
No comments