Jioni Njema; Chelsea wamkomalia Aguero # Martial out Perisic in # Hammers kumnasa Chicharito
LONDON- MABINGWA wa EPL, Chelsea, wameendelea kupambana
vikali ili kuhakikisha wanainasa saini ya mshambuliaji wa Manchester City,
Sergio Aguero (29) ili kuziba pengo la Diego Costa. Sky Sports.
Mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial (21) anaweza akatumiwa
kubadilishana na winga wa Inter Milan, Ivan Perisic (28). Gazzetta dello
Sport.
Kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny (27), amewasili katika jiji la Turin
kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya ili kujiunga na mabingwa wa Serie A,
Juventus kwa ada ya pauni milioni 10 (sh bilioni 29). Evening Standard.
Mmiliki wa
Chelsea, Roman Abramovich amesema hayupo tayari kulipa ada ya nyongeza
inayoongezeka kwenye usajili wa mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata (24)
na kusafisha njia ya mchezaji huyo kuelekea Italia. Star.
Manchester
United wamepanga kutoa pauni milioni 60 (sh bilioni 174), kama dau lao la
mwisho kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Tottenham, Eric Dier. Mirror.
Wagonga Nyundo
wa London, West Ham United, wanatarajiwa kukamilisha dili la kumsajili
mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Javier Hernandez kwa dau ambalo bado
halijawekwa wazi. Sun.
Manchester
City wamesafishiwa njia ya kumsajili winga wa Arsenal, Alexis Sanchez (28),
baada ya Bayern Munich ya Ujerumani kujitoa kwenye mchakato wa kumsajili
mshambuliaji huyo. Manchester Evening
News.
Mshambuliaji
wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic (35), amesema kuwa atasaini mkataba
mpya na United na kuwarudisha wanawe
kwenye akademi ya timu hiyo. Sun.
Klabu ya
Napoli ya Italia, imedaiwa kulipiga chini dau la pauni milioni 2.6 (sh bilioni
7.5) kutoka Manchester City, ili kumsajili Pepe Reina (34). Mirror.
Wageni wenyeji wa Ligi Kuu ya Uingereza, Newcastle United, wameripotiwa
kuweka mezani dau la pauni milioni 5 (sh bilioni 14.5), kwa ajili ya kumsajili
mshambuliaji wa Bordeaux, Diego Rolan (24). Chronicle.
Bosi wa Crystal Palace, Frank de Boer anaamini kuwa mshambuliaji wake,
Christian Benteke (26) ataendelea kubakia klabuni hapo licha ya kutakiwa na
wapinzani wao kwenye EPL, Chelsea na Everton. Evening Standard.
Kocha wa
Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo, Alexis
Sanchez hataondoka klabuni hapo kwani hauzwi. Wenger anategemea Sanchez ataweza
kuisaidia timu hiyo kurudi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao. Sky Sports.
Crystal Palace
wametenga dau la pauni milioni 16 (sh bilioni 46.4), kwa ajili ya kumsajili
beki wa Arsenal, Calum Chambers (22). Telegraph.
No comments