Header Ads

Asubuhi Njema; Morata kutua Chelsea # Liverpool yampandia Keita # Man United wamfuata Verratti



http://cdn.images.dailystar.co.uk/dynamic/58/photos/770000/620x/Alvaro-Morata-621537.jpg

LONDON- CHELSEA wamefikia makubaliano na Real Madrid, kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wao, Alvaro Morata (24) kwa dau lenye thamani ya pauni milioni 70 (sh bilioni 203). 
http://e0.365dm.com/16/08/16-9/20/diego-costa-chelsea-west-ham_3765670.jpg?20160815215603
Timu hiyo pia imeripotiwa kutaka dau la pauni milioni 44 (sh bilioni 127.6), kutoka Atletico Madrid kama ada ya kumuuza Diego Costa. Hata hivyo, Rais wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo amesema hawezi kutoa kiasi hicho. Independent.
https://img.bleacherreport.net/img/article/media_slots/photos/002/700/651/fd40d9416ebd1b19248f2c8f667ee295_crop_exact.jpg?h=533&w=800&q=70&crop_x=center&crop_y=top
Liverpool iko tayari kutoa pauni milioni 70 (sh bilioni 203), kama dau la kumsajili kiungo wa RB Leipzig ya Ujerumani, Naby Keita. Dau hilo linakuja baada ya dau lao la pili la pauni milioni 66 kukataliwa. Mirror.
http://img.bleacherreport.net/img/images/photos/003/538/660/hi-res-4966a29751464c0822b5a50f774e0ca0_crop_north.jpg?1445961530&w=630&h=420
Manchester United imejitosa mazima kwenye dili la kumsajili kiungo wa PSG ya Ufaransa, Marco Verratti (24) baada ya Muitaliano huyo kuingia mkataba na Mino Raiola ili awe wakala wake. Sun.
http://www.trbimg.com/img-5719608d/turbine/la-sp-sn-chicharito-to-play-for-mexico-in-copa-america-passing-up-olympics-20160421
West Ham wanatarajiwa kumsainisha muda wowote mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Javier Hernandez (29), kwa dau ambalo linadaiwa kuwa pauni milioni 13 (sh bilioni 37.7). Sky Sports.
http://i3.liverpoolecho.co.uk/incoming/article10328511.ece/ALTERNATES/s615/rossreact.jpg
Man United wanafuatilia kwa karibu hatima ya kiungo wa Everton, Ross Barkley (23) klabuni hapo, lakini wanatarajiwa kugonga mwamba kwani Barkley mwenyewe amesema anahitaji kujiunga na Tottenham Hotspurs. Standard.
https://cdn.vox-cdn.com/thumbor/Thmh148QLSSQvSZWfcKq-RCacm4=/0x37:3000x2037/1200x800/filters:focal(0x37:3000x2037)/cdn.vox-cdn.com/uploads/chorus_image/image/46760398/GettyImages-462650660.0.jpg
Wakongwe wa soka la Italia, AC Milan, wamesema kuwa mshambuliaji wao, Suso (23) ambaye anawindwa vikali na Tottenham Hotspurs, hauzwi. Talksport.
http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2017/0211/r179945_1296x729_16-9.jpg&w=738&site=espnfc
Inter Milan imewaambia Man United kuwa, dili lolote lenye nia ya kumtaka winga wao, Ivan Perisic (28) lazima limhusishe mshambuliaji Mfaransa, Anthony Martial (21) pamoja na pauni milioni 48 (sh bilioni 139.2). Independent.
http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2016/1027/r145768_1296x729_16-9.jpg&w=738&site=espnfc
Imebainika kuwa Manchester United na Chelsea zilikuwa zikifukuzia kimya kimya dili la kumsajili mshambuliaji wa Barcelona, Neymar (25) lakini walikwamishwa na kifungu kinachodai kuwa thamani ya mchezaji huyo ni pauni milioni 196 (sh bilioni 565.5). Mail.
http://cdn.images.dailystar.co.uk/dynamic/58/photos/249000/Lewis-Gibson-887249.jpg
Newcastle wamekubali ombi la Everton, ambao walikuwa wakimhitaji kinda wao Lewis Gibson (17). Everton wanataka beki huyo ajiunge na kikosi chao cha wachezaji wa under 23. Liverpool Echo.

No comments

Powered by Blogger.