Raila kuanika namna alivyoibwa kura leo

NAIROBI- KIONGOZI wa upinzani nchinI, Raila Odinga ambaye
alishindwa katika uchaguzi wa urais uliopita, ameliambia gazeti la Financial
Times la Uingereza kwamba leo atafichua ushahidi kuhusu namna alivyoibiwa kura.
“Tutauonyesha
ulimwengu wote, namna mfumo ulivyochezewa,” alisema Raila.
Raila ambaye
alikuwa akiwania urais kwa mara ya nne, alibainisha kwamba hatowania tena urais
na kuwataka Wakenya kujua kilichofanyika wakati wa uchaguzi huo.
“Sio suala
la kuwa mbifasi, sio suala kuhusu Raila Odinga, sitawania urais
tena......tunataka Wakenya kujua kile kilichofanyika, na kile ambacho ulimwengu
haujui kinafanyika,” alisema Raila.
Raila amedai
kwamba, wadukuzi waliingilia kompyuta za tume ya Uchaguzi na kuweka hesabu
ambazo zilimpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta. Hata hivyo, madai hayo yamepuuzwa
na tume ya uchaguzi.
BBC
No comments