Header Ads

Asubuhi njema; Bakayoko kutua muda wowote Chelsea # Mourinho amtaka Dier wa Spurs # Wenger kumbakiza Sanchez

https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/03/653597506.jpg?w=748&h=498&crop=1


LONDON- KWA mujibu wa vyanzo vya kuaminika vya Sky Sports, Chelsea wapo karibu zaidi kumsainisha kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko (22) na muda wowote ataweza kutua London kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.
Bakayoko anatarajiwa kufanyiwa vipimo hivyo na kusafiri na timu kwenda Singapore, Jumatatu ijayo. Inadaiwa kuwa dau lililokubaliwa ni kati ya pauni milioni 35-40 (sh bilioni 101 au 120). Sky Sports.
http://e1.365dm.com/15/11/16-9/20/eric-dier-tottenham-uefa-europa-league_3373322.jpg?20151105215355
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, ameutaka uongozi wa klabu hiyo kupeleka dau la pauni milioni 60 (sh bilioni 174) kwa Tottenham Hotspurs ili kumsajili kiungo wao, Eric Dier (23). Mirror.
http://www.thegunners247.uk/resources/as7980.jpg?timestamp=1439822344007
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa anategemea ataendelea kupata huduma ya mchezaji wake, Alexis Sanchez (28) ambaye bado hajakubali kusaini mkataba mpya na klabu hiyo kutokana na kudaiwa kutaka kuhamia Manchester City. Independent.
https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/01/624810664.jpg?w=620&h=412&crop=1
Manchester United bado hawajafikia makubaliano rasmi na Inter Milan, kuhusiana na usajili wa Ivan Perisic (28), lakini dili hilo linalodaiwa kuwa ni pauni milioni 50 (sh bilioni 145) linatarajiwa kukamilika muda wowote wiki ijayo. Independent. 
http://cdn.empireofthekop.com/wp-content/uploads/2017/06/Van-Dijk.jpg
Arsenal wanadaiwa kujitosa rasmi kwenye mpambano wa kumnyakua beki wa kati wa Southampton, Virgil van Dijk (26) ambaye anatakiwa na klabu za Liverpool na Manchester City. The Sun.
http://cdn.images.express.co.uk/img/dynamic/galleries/x701/98069.jpg
Roma ya Italia imeweka wazi mpango wao wa kumtaka kwa mkopo wa msimu mzima mshambuliaji wa Man United, Anthony Martial (21) lakini United hailitaki dili hilo. Mirror.
http://cdn.caughtoffside.com/wp-content/uploads/2015/04/James-Rodriguez-Real-Madrid.jpg
James Rodriguez ameiambia Real Madrid kuwa anataka ajue mustakabali wa maisha yake ya soka klabuni hapo, kutokana na kutakiwa na Man United na Chelsea. Hata hivyo, inadaiwa Madrid wanataka pauni milioni 62 () kama ada yake. Daily Mail.
http://i4.manchestereveningnews.co.uk/incoming/article10827865.ece/ALTERNATES/s615/JS81722468.jpg
Leicester City wamekubaliana na Man City kuhusu vigezo vya msingi bya usajili wa mshambuliaji wao kinda, Kelechi Iheneacho (20), lakini haijawekwa wazi ni kiasi gani wamewapatia wababe hao wa Manchester. Sky Sports.
https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/03/654435046.jpg?w=748&h=465&crop=1
Licha ya kuendelea kubakia katika viwanja vya mazoezi vya Carrington, Manchester, akielekea kupona maumivu ya goti, Zlatan Ibrahimovic bado hajapewa mkataba na Man United wamedaiwa kutokuwa tayari kumwongezea mkataba mshambuliji huyo. Star.
http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2016/0426/r77611_1296x729_16-9.jpg&w=738&site=espnfc
Manchester City imedaiwa kuwa ni moja kati ya klabu nne za Ulaya, ambazo ziko tayari kulipa pauni milioni 27 (sh bilioni 78.3) kama ada ya uhamisho ya mshambuliaji wa Real Sociedad, Inigo Mrtinez (26). Marca.

No comments

Powered by Blogger.