Header Ads

Asubuhi Njema; Bakayoko kusaini miaka 5 Chelsea # Arsenal watoa £45 kwa Lemar # Matic aitaka United # Hazard awaita Madrid



http://images.performgroup.com/di/library/GOAL_INTERNATIONAL/5e/e1/tiemoue-bakayoko_1b2jafsy5y5ns19cq553kqc09k.jpg?t=209384681&w=620&h=430

LONDON- Chelsea wamefikia makubaliano na klabu ya Monaco, kuhusu usajili wa kiungo wao, Tiemoue Bakayoko (22), kwa dau la pauni milioni 40 (sh bilioni 116). Bakayoko atasaini mkataba wa miaka 5 muda wowote kuanzia sasa. RMC.
https://d13csqd2kn0ewr.cloudfront.net/uploads/image/file/163983/cropped_REU_2307078.jpg?ts=1457125040
Klabu ya Arsenal, inaamini kuwa ofa yao ya pauni milioni 45 (sh bilioni 130.5) ni nzuri na wanatarajia kuwa itakubaliwa na Monaco, kwa ajili ya uhamisho wa winga Thomas Lemar. Daily Mail.
http://talksport.com/sites/default/files/styles/just_scale/public/field/image/201705/gettyimages-689628226.jpg?itok=Szc5cw_t
Chelsea wameelezwa kwamba, wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Piere-Emerick Aubameyang kwa ada ya pauni milioni 60 (sh bilioni 174), baada ya miamba ya soka la China, Tianjin Quanjian kujitoa kwenye usajili wa mchezaji huyo mwenye miaka 28. Daily Mail.
http://images.performgroup.com/di/library/goal_uk/fd/c7/hd-olivier-giroud-arsenal_6su0y9ukgnl9z3ck0ati7gev.jpg?t=316600783&w=620&h=430
Baada ya kuona kuwa straika wao mkali, Piere-Emerick Aubameyang anaweza kuondoka muda wowote, Borussia Dortmund wamejitosa kwenye mchakato wa kumsajili Olivier Giroud wa Arsenal, ambaye pia anatakiwa na West Ham. Daily Mail.
http://s.newsweek.com/sites/www.newsweek.com/files/2016/11/07/eden-hazard.jpg
Winga wa Chelsea, Eden Hazard (26) amemtaka kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane kuamua kuhusu hatima ya usajili wake kwenda kwa mabingwa hao wa Ulaya msimu huu. Daily Express.
http://cdn.empireofthekop.com/wp-content/uploads/2017/06/Van-Dijk.jpg
Mchezaji wa zamani wa Liverpool, Danny Murphy, amesema klabu hiyo iko mbioni kukamilisha usajili wa mlinzi wa kati wa Southampton, Virgil van Dijk (26) kwa dau ambalo halijawekwa wazi. Sport360.
http://i2.mirror.co.uk/incoming/article10692845.ece/ALTERNATES/s1200/Manchester-Uniteds-Marouane-Fellaini-in-action-with-Chelseas-Nemanja-Matic.jpg
Baada ya kufanikiwa kumpata kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko, sasa kocha wa Chelsea, Antonio Conte, anatarajiwa kumuweka sokoni kiungo wake,Nemanja Matic. Mserbia huyo amekuwa akifanya mazoezi peke yake na anadaiwa kusema kuwa anataka aungane na Jose Mourinho huko Man United. Daily Telegraph.
https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/07/nintchdbpict000324641632.jpg?strip=all&w=960&quality=100
Chelsea wanatarajiwa kuipiku Juventus kwenye usajili wa beki, Danilo kutoka Real Madrid kwa dau la pauni milioni 28 (sh bilioni 81.2). Daily Miror.


No comments

Powered by Blogger.