Maporomoko ya mlima na mafuriko yaua watu 300 Sierra Leone

FREE TOWN- WATU zaidi ya 300 wanahofiwa kupoteza maisha,
kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko mjini hapa, na huenda idadi hiyo
ikaendelea kuongezeka.
Inahofiwa
kwamba, miili zaidi ya watu waliofariki dunia kutokana majanga hayo, iko chini
ya vifusi. Jitihada za uokoaji, zilisitishwa kwa muda baada ya giza kuingia.
Rais Ernest
Bai Koroma amesema kupitia televisheni ya taifa kwamba, vituo vya dharura
vimewekwa ili kukabiliana na kile alichokiita janga la taifa.
Shirika la
Msabala mwekundu, limesema inakadiriwa zaidi ya watu 300,000 wamepoteza makazi.
Eneo
lililoathirika zaidi ni wilaya ya Regent, iliyopo pembezoni Freetown baada ya
mlima uliojaa maji kuporomoka.
BBC
No comments