Header Ads

Modric aionya Real Madrid kwa Rodriguez # Chlesea yatoa £70m kwa Morata # Sanchez na Bellerin waondolewa ‘list’ ya Arsenal



https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/06/nintchdbpict000268053310.jpg?strip=all&w=960&quality=100

MANCHESTER- KIUNGO Mshambuliaji wa Real Madris, Luka Modric amesema kitendo cha klabu hiyo kutaka kumuachia mshambuliaji wake, James Rodriguez kujiunga na Manchester United kitakuwa ni kosa kubwa.
Mcolombia huyo amekuwa akiitaka Real Madrid imwache akatafute timu nyingine ambayo atakuwa na uhakika wa kuwepo kwenye kikosi cha kwanza na kucheza mara kwa mara. 
https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/01/nintchdbpict000292291069.jpg?strip=all&w=960
Chelsea wanapanga kutoa kitita cha pauni milioni 70 (sh bilioni 203), kama ada ya uhamisho wa mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata.
Hayo yanajiri muda mfupi, baada ya Man United kuwapora windo lao kutoka Everton, Romelu Lukaku. Morata amekuwa akitakiwa kwa muda mrefu na Man United na hivyo kuilazimu Chelsea kuongeza umakini kwenye usajili wake, ili wasije wakaporwa tena.
http://images.performgroup.com/di/library/GOAL/b5/d6/diego-costa_83x4cxdr1a9m1q3g35jiqv55x.jpg?t=-1495762189
Licha ya kuwepo kwa habari kuhusu mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa kutotakiwa na kocha wa timu hiyo, Antonio Conte kwenye kikosi chake, mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kurejea mazoezini leo.
Straika huyo alisema hivi karibuni kwamba, Conte alimtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) ukimjulisha kuwa hatakiwi tena klabuni hapo licha ya kufunga magoli 20 msimu uliopita na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.
http://images.performgroup.com/di/library/GOAL/c2/9a/alexis-sanchez-arsenal_xfqojqay0qtc1d6lndjkhuuay.jpg?t=450514947
Kikosi cha timu ya Arsenal, kimeruka kwenda Australia kwenye ziara bila ya wachezaji wake wawili, Alexis Sanchez na Hector Bellerin ambao wameongezewa muda wa kupumzika.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa wachezaji hao wanabaki ili kukamilisha madili yao ya usajili. Pia, wachezaji wapya wawili, Alexandre Lacazzette na Sead Kolasinac, wanatarajiwa kucheza michezo yao ya kwanza na timu yao mpya.
http://futebolatino.com.br/arqsist/uploads/2016/04/Paulinho.jpg
Windo la klabu ya Barcelona, Paulinho, amedaiwa kueleza kuwa atakutana na Rais wa klabu yake ya Guangzhou Evergrande ili kufanya mazungumzo yatakayomuwezesha kuondoka klabuni hapo na kujiunga na wababe hao wa Hispania.
Habari zote na Sky Sports

No comments

Powered by Blogger.