Ulinzi waimarishwa Bomas Kenya
NAIROBI- ULINZI umeimarishwa katika eneo la Bomas ambalo
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC), imekuwa ikilitumia kuandaa na
kutangaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika kote nchini Agosti 8.
Hali hiyo
inakuja, ikiwa ni IEBC inatarajiwa kutangaza rasmi matokeo ya urais muda wowote
kuanzia sasa.
Leo asubuhi,
IEBC ilipokea jumla ya fomu 270 kati ya 290 za 34b, na inaendelea kusubiri fomu
20 za aina hiyo ambazo zinatarajiwa kuwasilishwa muda wowote hapo Bomas.
Tume hiyo imesema
kuwa, mara baada ya fomu hizo zilizobaki kuwasili na kuhakikiwa na maofisa wa
IEBC na mawakala wa wagombea, ndipo itatangaza rasmi matokeo ya urais ambayo
yamekuwa yakisubiriwa.
Awali, NASA
ambao ni Muungano wa Upinzani nchini, ilidai kuwa mfumo wa uchakataji matokeo
wa IEBC ulidukuliwa na wadukuzi ambao walipindua kura za Raila Odinga.
Pia, NASA
waliitaka tume hiyo kumtangaza Raila kuwa ndiye mshindi kutokana na kudai kuwa
alipata kura nyingi zaidi ya mpinzani wake, Rais Uhuru Kenyatta wa Jubilee.
Hata hivyo,
madai hayo ya NASA yalitupiliwa mbali na Mwenyekiti wa IEBC, Wefula Chebukati
ambaye alidai kuwa wadukuzi hawakufanikiwa kudukua mfumo huo licha ya kujaribu
kufanya hivyo.
The
Standard Digital.
No comments