Coutinho kuikosa Watford kesho

LIVERPOOL- LIVERPOOL wanatarajiwa kucheza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu (EPL) kesho, kwa
kuwakabili Watford bila ya kiungo wao mahiri, Philippe Coutinho ambaye ana
maumivu ya mgongo.
Majogoo hao wa Anfield, wataikosa huduma ya mchezaji huyo baada ya
daktari wa timu hiyo kuthibitisha kuwa ana maumivu ya mgongo ambayo
yanatarajiwa kumuweka nje kwa muda ambao hakuutaja.
Coutinho, amekuwa nguzo muhimu kwa Liverpool na kocha Jurgen Klopp
ambaye amekataa kata kata kumuuza kwenda Barcelona licha ya kupewa dau la pauni
milioni 100 (sh bilioni 290).
Sky Sports.
No comments