Arsenal na Leicester City kukata utepe EPL leo
LONDON- MCHEZO wa kwanza wa Ligi Kuu nchini maarufu EPL,
unatarajiwa kuchezwa leo ambapo Arsenal watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani
Emirates, kuwakaribisha Leicester City.
Mchezo huo
unaotarajiwa kuanza majira ya saa 9:45 kwa saa za Afrika Mashariki, utakuwa
mkali kutokana na namna timu hizo zinavyokuwa na upinzani.
Arsenal ambao
wamewasajili Alexandre Lacazette na Sead Kolasinac, wanatarajiwa kuingia
uwanjani wakiwa na kumbukumbu za kushinda mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya
Chelsea kwa penati baada ya kutoka sare ya 1-1 katika dakika 90 za mchezo.
Vikosi vinatarajiwa
kuwa kama ifuatavyo;
Arsenal;
Petr Cech, Rob Holding, Per Mertesacker, Nacho Monreal, Hector Bellerin, Granit
Xhaka, Mohamed Elneny, Alex Iwobi, Alexandre Lacazette na Danny Welbeck.
Arsenal watatumia mfumo wa 3-4-3
Leicester
City; Kasper Schmeichel, Danny Simpson, Wes Morgan, Harry Maguire, Christian
Fuchs, Mathew James, Onyinye Ndidi, Riyad Mahrez, Shinji Okazaki, Marc
Albrighton na Jamie Vardy. Mfumo wao unatarajiwa kuwa 4-2-3-1.
Utabiri wangu
Mchezo wa leo unaweza ukaisha kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa bao 2-1.
Utabiri wangu
Mchezo wa leo unaweza ukaisha kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa bao 2-1.
No comments