Top 6 ya timu za Uingereza zinazopiga fedha kupitia udhamini wa jezi

Katika Ligi Kuu ya Uingereza maarufu EPL, timu
nazo haziko nyuma katika kuchangamkia biashara hiyo na ifuatayo ni orodha ya
timu zinazopiga mkwanja mrefu kupitia udhamini huo wa kwenye mashati.
1. Manchester United
Dili la Manchester
United na kampuni ya utengenezaji magari ya Chevrolet, ni moja kati ya madili
yenye thamani ya juu kwani lina thamani ya pauni milioni 47 (sh bilioni 136.3)
kwa mwaka.
Mbali na
hilo, kwa sasa United wako katika mazungumzo na kampuni inayomiliki mtandao wa
kijamii wa Tinder, kwa ajili ya kuweka nembo yao kwenye sehemu ya mikono ya
jezi ya Manchester United.
Mdhamini Mkuu (kwenye shati kifuani): Chevrolet
Thamani ya dili: Pauni milioni 47 kwa msimu hadi 2021
Mabegani mwa jezi: Wako kwenye mazungumzo na Tinder App
Thamani ya
dili: Linatarajiwa kuwa zaidi ya pauni milioni 10 (sh bilioni 29).
2. Chelsea
Chelsea wamefuata
nyayo za Manchester City, ambao walikubali kuingia mkataba wa kuweka udhamini
wa kampuni nyingine katika sehemu ya mikono chini ya bega kwenye jezi zao.
Chelsea inadhaminiwa
na Yokohama Tyres, ambao ni watengenezaji wa matairi dili hilo likiwa na
thamani ya pauni milioni 40 (sh bilioni 116), lakini imeingia mkataba na
kampuni na Alliance Tyres ili waweke nembo kwenye sehemu ya chini ya mabega
kwenye jezi zao.
Mdhamini Mkuu: Yokohama Tyres
Thamani ya dili: Pauni milioni 40 kwa msimu hadi 2020
Mabegani mwa jezi: Alliance Tyres
Thamani ya dili: Pauni milioni 8 million kwa msimu wa 2017/18.
3. Manchester City
Licha ya
Etihad Airways kuwa mdhamini mkuu wa Manchester City, katika dili lenye thamani
ya pauni milioni 35 (sh bilioni 101.5) lakini timu hiyo ilikuwa ya kwanza kuwa
na ufadhili kwenye sehemu ya mabegani mwa jezi wanazovaa.
Nexen Tire, ambao
ni watengenezaji wa matairi kutoka Korea Kusini ndiyo waliokuwa wa kwanza
kuanzisha udhamini huo. Udhamini huo una thamani ya pauni milioni 7 (sh bilioni
20.3) kwa mwaka.
Mdhamini Mkuu: Etihad
Airways
Thamani ya dili: Pauni milioni 35 kwa mwaka hadi 2021
Mabegani mwa jezi: Nexen Tire
Thamani ya mkataba: Pauni milioni 7 million kwa mwaka.
4. Tottenham HotSpurs
AIA
(American Insurance Association) wanawalipa Tottenham pauni milioni 35 (sh
bilioni 101.5) kwa mwaka, kama sehemu ya mkataba wao wa udhamini.
Spurs bado hawajatangaza
mdhamini wa sehemu ya mabegani kwenye jezi zao kama walivyofanya Man City na
Chelsea.
Mdhamini Mkuu: AIA
Thamani ya dili: Pauni milioni 35 kwa mwaka hadi 2022
Mabegani mwa jezi: Hakuna kwa sasa.
5. Liverpool
Liverpool
wanajivunia kuwa na Standard Chartered, ambao wamekuwa wadhamini wao wakuu
tangu mwaka 2010. Dili lao lina thamani ya pauni milioni 30 (sh bilioni 87)
ambazo ziko sawa na zile wanazolipwa Arsenal na Fly Emirates.
Tofauti ya
Liverpool na Arsenal ni kwamba, majogoo wa Anfield wanaingiza ziada ya pauni
milioni 5 (sh bilioni 14.5) kwa mwaka kutoka kwa Western Union ambao wameweka
nembo yao mabegani mwa jezi za Liverpool. Dili hilo litakuwa la miaka mitano.
Mdhamini Mkuu: Standard Chartered
Thamani ya dili: Pauni milioni 30 kwa mwaka hadi 2019
Mabegani mwa jezi: Western Union
Thamani ya dili: Pauni milioni 5 kwa mwaka
hadi 2022
6. Arsenal
Udhamini wa
muda mrefu wa Fly Emirates kwa Arsenal, unaifanya klabu hiyo kushika nafasi ya
tano kwa kuweka kibindoni pauni milioni 30 (sh bilioni 87) kwa mwaka.
Hadi sasa
hakuna mkataba wala mazungumzo yoyote na kampuni kwa ajili ya kuweka nembo
mabegani.
Mdhamini Mkuu: Fly Emirates
Thamani ya dili: Pauni milioni 30 kwa mwaka
hadi 2019
Mabegani mwa jezi: Hakuna kwa sasa
Chanzo; Mirror
No comments