Coutinho aomba kuondoka Liverpool

LIVERPOOL-
KWA mujibu wa mtandao wa shirika la habari la Sky Sports, mchezaji mahiri wa
Liverpool, Philippe Coutinho (25) amewasilisha rasmi hati ya kuomba kuondoka
klabuni hapo.
Sky Sports
imeeleza kuwa habari hizo wamepewa na mmoja wa watu wa familia ya Coutinho,
ambaye alidai kwamba; “Coutinho amejaribu kwa kadri awezavyo kutafuta kuondoka
kwa njia njema, na ya urafiki lakini ameshindwa kabisa.”
“Anaipenda
sana Liverpool na mashabiki wake, lakini kama ilivyokuwa kwa Steven Gerrard na
Luis Suarez hawakuweza kuondoka kirafiki. Liverpool huwa hairuhusu wachezaji
wake kuondoka kwa njia ya kirafiki.”
Kwa upande
mwingine, Stock City imekamilisha usajili wa beki wa Uholanzi na Porto, Bruno
Martins Indi kwa ada yenye thamani ya pauni milioni 7 (sh bilioni 20.3). Sky Sports.
No comments