Tetesi Leo; Chelsea wamtega Costa # Man City watoa £60 kwa Sanchez # Arsenal wamtaka Asensio
LONDON- MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu nchini (EPL),
Chelsea, wanadaiwa kumpa masharti kadhaa ya kutimiza mshambuliaji wao anayetaka
kuuzwa, Diego Costa (28) ili apate kuondoka klabuni hapo. Guardian.
Manchester City wanaamini jaribio lao lenye thamani ya pauni milioni 60
(sh bilioni 174), litaweza kuishawishi Arsenal wawauzie mshambuliaji wao raia
wa Chile, Alexis Sanchez (28) kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la msimu
huu. Telegraph.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amekwaruzana na uongozi wa timu hiyo
kuhusiana na idadi ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa. Muitaliano huyo anataka
kuwasainisha haraka wachezaji wazoefu na wanaouzwa bei chee. Times.

Barcelona wamesema dau lao la pauni milioni 90 (sh bilioni 261), kama ada
ya uhamisho wa Ousmane Dembele (20) limekubaliwa na klabu ya Borussia Dortmund
ya Ujerumani. Daily Express.

Nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson amesema atajaribu kadri awezavyo
kumshawishi mchezaji mwenzake Philippe Coutinho (25), kubaki klabuni hapo na
kuipuuza ofa ya Barcelona. Daily Mirror.
Kiungo mshambuliaji wa Real Madrid, Marco Asensio (21) ametaka kikao cha
dharura baina yake na uongozi wa timu hiyo, baada ya kupokea ofa ya Arsenal. Sun.

Juventus wamesema wanavutiwa na mpango wa kumsajili kiungo wa Arsenal,
Jack Wilshere (25), ambaye hatima ya maisha yake ya mpira yako shakani
Emirates. Daily Mirror.
Beki mahiri wa Southampton, Virgil van Dijk (26) huenda akajiunga na
aidha Chelsea au Manchester City kuliko Liverpool ambayo imekuwa ikimtaka. Hata
hivyo, Southampton wanataka pauni milioni 70 (sh bilioni 203) kama ada ya
uhamisho. Yahoo.
Chelsea wanaamini kuwa wanaweza kumnasa winga wa Arsenal, Alex
Oxlade-Chamberlain (23) kwa ada ya pauni milioni 35 (sh bilioni 101.5) kabla ya
kufungwa kwa dirisha la usajili la msimu huu. Evening Standard.
Maofisa wa Tottenham Hotspurs wamesafiri jana kwenda Amsterdam, kwa ajili
ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Ajax ili wamsajili mlinzi wao wa kati,
Davinson Sanchez (21). Ajax wanadai beki huyo anauzwa pauni milioni 36 (sh
bilioni 104.4). Sky Sports.
No comments