Mwakyembe kuongoza mapokezi ya Simbu leo
DAR ES SALAAM- WAZIRI wa
Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dk Harrison Mwakyembe, leo atawaongoza
wadau mbalimbali wa michezo kumlaki Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya shaba
katika michuano ya dunia, Uingereza.
Simbu ambaye alitwaa
medali hiyo katika mbio za London Marathon, anatarajiwa kuwasili mchana wa leo
na wenzake katika kundi la kwanza la wanariadha wa Tanzania waliokuwa
wakishiriki mashindano hayo.
No comments