Hazard na Bakayoko waanza mazoezi Chelsea
LONDON- HABARI njema kwa mashabiki wote wa mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu England (EPL), ni kwamba mshambuliaji wao machachari, Eden
Hazard amerudi mazoezini baada ya kuwa nje kwa miezi miwili.
Hazard alionekana
mazoezini leo, huku akionekana mwenye furaha na kuashiria kuwa amepona tatizo
la kifundo cha mguu (ankle) ambalo lilimpata akiwa katika majukumu ya
kuiwakilisha timu yake ya taifa, Ubelgiji.
Licha ya Hazard
ambaye aliumia mwezi Juni mwaka huu kurudi mazoezini, mshambuliaji mwingine wa
timu hiyo, Pedro Rodriguez ameendelea kuwa nje kutokana na tatizo la kifundo
cha miguu.
Kwa upande
mwingine, kiungo mpya wa timu hiyo, Tiemoue Bakayoko alionekana akifanya
mazoezi mepesi ambayo yanamaanisha kuwa anaendelea kupona taratibu baada ya
kufanyiwa upasuaji wa goti.
Bakayoko
Mwishoni mwa
wiki iliyopita, Chelsea walionekana kupwaya zaidi baada ya kukumbana na kipigo
cha bao 3-2 kutoka kwa Burnley.
Daily Mail.
No comments