Tetesi Asubuhi; Barcelona waigwaya Liverpool # Chelsea wakataliwa Sandro # Man United wamuota Perisic

LONDON- MKURUGENZI wa Michezo wa Barcelona, Robert
Fernandez amesema itakuwa vigumu kumsajili kiungo wa Liverpool, Philippe
Coutinho (25), kwa kuwa hana kipengele cha kumruhusu kuondoka. Hata hivyo,
wamesema watapambana hadi dirisha la usajili litakapofungwa. Liverpool Echo.

Kwa mara nyingine tena, Chelsea imeendelea kugonga
mwamba kwenye mpango wao wa kumsajili beki wa Juventus na Brazil, Alex Sandro
(26), baada ya ofa yao ya pauni milioni 63 (sh bilioni 182.7) kukataliwa. Mirror.
Manchester
United bado hawajakata tamaa kuhusiana na mpango wao wa kumsajili winga wa
Inter Milan, Ivan Perisic (28), licha ya United kutoa pauni milioni 39 (sh
bilioni 113.1). Mirror.

Manchester City wako tayari kutoa pauni milioni 22
(sh bilioni 63.8), kwa ajili ya kumsajili beki wa West Brom, Jonny Evans (29),
baada ya dau lao la kwanza kukataliwa. Evans anatarajiwa kulipwa pauni 75,000
(sh milioni 217.5) kwa wiki Etihad. Mirror.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Borussia Dortmund amesema Barcelona hawako karibu kukamilisha
usajili wa winga wao, Ousmane Dembele, kwani hawajafikia matakwa ya klabu hiyo ya
Signal Iduna Park. Kicker.
Tottenham wako karibu kuinasa saini ya beki wa kati
wa Ajax na Colombia, Davinson Sanchez (21), kwa ada ya pauni milioni 28 (sh
bilioni 81.2) na ongezeko la pauni milioni 14 (sh bilioni 40.6). Independent.

Mshambuliaji mahiri wa Chelsea, Diego Costa (28)
amesema hatarudi Stamford Bridge kamwe na anajiandaa kujiunga na Atletico
Madrid. Mchezaji huyo kwa sasa yuko kwao Brazil. Telegraph.

Beki wa Arsenal na Brazil, Gabriel (26) yuko karibu
kukamilisha uhamisho wa kwenda Valencia, kwa ada yenye thamani ya pauni milioni
10 (sh bilioni 29). Evening Standard.

Everton inapanga kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa
Chelsea, Diego Costa (28) ambaye kocha wa Chelsea, Antonio Conte alimwambia
hayupo kwenye mipango yake. Sun.
PSG
wanasema bado wana mpango wa kumsajili kiungo wa Monaco na Brazil, Fabinho
(23). L’Equipe.
Kiungo
wa PSG, Blaise Matuidi (30) amekamilisha uhamisho wake wa kwenda Juventus
lakini bado klabu hizo hazijakubaliana kuhusu ada. Kocha wa PSG, Unai Emery
hataki kumuuza mchezaji huyo. Le
Parisien.
Uongozi
wa Fiorentina umemwambia mshambuliaji wao raia wa Croatia, Nikola Kalinic (29),
atapigwa faini kutokana na kutoripoti mazoezini jana. Kalinic anawindwa na AC
Milan. Sun.
No comments