Mkulima kumzawadia ng’ombe wake wa pekee Rais Kenyatta
THARAKA- MKAZI mmoja wa kijiji cha Nkondi, amepanga kusafiri umbali wa kilometa 500 hadi kufika Ikulu ya Kenya jijini Nairobi, kwa ajili ya kumpa zawadi Rais Uhuru Kenyatta.
Mwanaume huyo,
Duncan Mutiria mwenye umri wa miaka 40, amesema anapanga kutembea umbali huo
mrefu ili kumpa Rais Kenyatta zawadi ya ng’ombe dume wa pekee aliyenaye.
“Ninataka
kwenda kumshukuru Rais Kenyatta. Nina watoto wawili wa kike, ambao sasa
wataweza kwenda shule na kusoma bure bwerere na hiyo ni kwa ukarimu wa chama
cha Jubilee,” alisema Mutiria.
Mutiria pia
aliongeza kuwa, atamshukuru kwa kitendo chake cha kuanza shughuli za ujenzi wa
barabara za kuiunganisha Tharaka na maeneo mengineyo ya nchi.
“Kwa muda
mrefu tulitengwa na tawala nyinginezo, lakini Serikali ya Uhuru imekuwa njema
kwetu. Amekuja kututembelea kwa kutumia barabara zisizo na madaraja, na njia
mbovu kabisa ambazo hazikuwahi kutumiwa na viongozi wengine,” alisema Mutiria.
Mkulima huyo
alisema amefurahi zaidi, kwani watoto wake ambao wapo darasa la nane
watanufaika na mpango wa elimu bure katika kupata elimu yao ya sekondari.
“Ndiyo maana
nimepanga kumzawadia ng’ombe wangu wa pekee Rais Kenyatta,” alisema Mutiria
ambaye amepanga kuianza safari yake Jumapili ya Agosti 20.
Katika safari
hiyo ya aina yake, Mutiria ataambatana na wenzake wawili kwa ajili ya kumsaidia
kubeba chakula cha ng’ombe huyo. Pia, aliongeza kuwa mtoto wake mmoja wa kike
ataambatana naye kwa ajili ya kwenda Ikulu kumshukuru Rais Kenyatta.
“Ninawaomba
viongozi wa Tharaka wanisaidie ili nionane na Rais Kenyatta, iwapo nitanyimwa
kuonana naye” alisema Mutiria.
The Star.
No comments