Rais wa Algeria amfuta kazi Waziri Mkuu

ALGIERS- RAIS
Abdelaziz Bouteflika amemfuta kazi Waziri Mkuu, Abdelmadjid Tebboune, ambaye
aliteuliwa na kudumu katika nafasi hiyo kwa muda usiozidi miezi mitatu.
Hakuna
sababu zilizotajwa za kuondolewa kwake kazini, lakini hatua hiyo imekuja siku
kadhaa, baada ya Rais kumtumia barua kali Tebboune kutaka mabadiliko ya sera.
Tayari Waziri
Mkuu mpya ametajwa kuwa ni Ahmed Ouyahia, ambaye alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Rais.
BBC
No comments