Nahodha wa Mexico awekewa vikwazo Marekani
MEXICO CITY-
SERIKALI ya Marekani imemuorodhesha mchezaji wa mpira wa miguu na nahodha wa
timu ya taifa ya Mexico, Rafael Marquez (38) kama mmoja wa watu 22 waliowekewa
vikwazo na taifa hilo kutokana na dawa za kulevya.
Mamlaka za
Marekani, zimeeleza kuwa Marquez amekuwa ni mmoja kati ya watu wenye mahusiano
ya karibu na mmoja wa mfanyabiashara wa dawa hizo nchini, Raul Flores Hernandez
pamoja na magenge ya Sinaloa, na Jalisco New Generation Gang yanayojihusisha na
dawa hizo.
“Raul Flores
Hernandez amekuwa akifanya kazi hiyo ya dawa za kulevya kwa miongo mingi, kutokana
na mahusiano yake na watu na magenge mengine. Anawatumia marafiki zake kuficha
biashara zake,” ilisema taarifa ya John E. Smith ambaye ni Mkurugenzi wa
Kitengo cha Mali za Nje katika ofisi ya Hazina ya Marekani.
DW
No comments