Mawakala wapitia fomu za matokeo usiku kucha Kenya






NAIROBI- WAKATI
matokeo rasmi yakisubiriwa kwa hamu zaidi, usiku wa kuamkia leo ulikuwa ni
usiku uliotawaliwa na shughuli nyingi hususan katika kituo cha taifa cha
kujumlishia matokeo ya uchaguzi maarufu Bomas.
Maajenti wa
vyama vya siasa, walikuwa wakikagua Fomu 34A za matokeo kutoka vituo vya
kupigia kura katika sehemu maalum.
Mgombea wa
upinzani, Raila Odinga alikuwa amelalamika awali kwamba IEBC ilikuwa ikitangaza
matokeo bila kutoa fomu hizo. Tume hiyo baadaye ilitoa fomu hizo.



Kufikia sasa
ni vituo 1,200 pekee kati ya 40,883 ambavyo havijawasilisha matokeo. Tume ya
uchaguzi imeahidi kutoa maelezo kuhusu matokeo yaliyo kwenye fomu
zilizopokelewa Bomas baadaye leo.
Kwa upande
mwingine, IEBC imekanusha vikali madai yote yaliyotolewa na Raila jana kwamba mtandao
wa tume hiyo uliingiliwa (kudukuliwa) na wadukuzi na kubadilisha matokeo.
BBC
No comments