Asubuhi Yetu; Mourinho awataka Rose na Perisic # PSG wamkomalia Mbappe # Barcelona wamng’ang’ania Coutinho

MANCHESTER- KOCHA wa Manchester
United, Jose Mourinho
amesema ameshauambia uongozi wa klabu hiyo ufanye haraka usajili wa beki wa
pembeni wa Tottenham Hotspurs, Danny Rose (27) na winga wa Inter Milan, Ivan
Perisic (28). Manchester Evening News.
Paris
St-Germain (PSG) wako katika hatua za mwisho za kumsajili mshambuliaji kinda wa
Monaco, Kylian Mbappe (18) kwa dau la pauni milioni 163 (sh bilioni 472.7). PSG
pia imeweka mezani ofa nzuri kwa Monaco, kwa ajili ya kiungo wao, Fabinho (23).
Daily Record.
Barcelona
wanatarajiwa kurudi kwa mara ya nne mezani mwa Liverpool, baada ya dau lao la
tatu la pauni milioni 90 (sh bilioni 261) kwa ajili ya kumsajili Philippe
Coutinho (25) kukataliwa Anfield. Daily Mail.
Kwa
mujibu wa vyanzo vya kuaminika kutoka Ufaransa, endapo Kylian Mbappe (18)
ataondoka Monaco, basi klabu hiyo italazimika kumsajili mshambuliaji wa AC Milan,
Carlos Bacca (30). Sun.
Chelsea
imetoa pauni milioni 35 (sh bilioni 101.5) kwa Arsenal, kama ada ya kumsajili
winga wa timu hiyo Alex Oxlade-Chamberlain (23) aliyebakiza mwaka mmoja kwenye
mkataba wake klabuni hapo. Daily Star.
Arsenal
wameeleza kuwa wanahofia mshambuliaji wao raia wa Chile, Alexis Sanchez (28)
huenda akaanzisha tena harakati zake za kutaka kuondoka klabuni hapo. Daily Mirror.

Inadaiwa
kuwa winga wa Chelsea na Brazil, Wilian (29) amefanya mazungumzo na Manchester
United, kwa ajili ya kujiunga tena na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho
ambaye awali walifanya kazi wote Stamford Bridge. Goal.

Beki
wa pembeni wa Tottenham anayewindwa na Manchester United, Danny Rose (27)
ameitaka klabu yake kutumia fedha kusajili wachezaji lakini si wale ambao
itakupasa uanze kutumia mtandao wa Google kutafuta huyo ni nani. The Sun.

West
Ham wanapanga kutoa pauni milioni 25 (sh bilioni 72.5) kwa Sporting Lisbon ya
Ureno, kama ada ya uhamisho wa kiungo mahiri wa timu hiyo, William Carvalho
(25). Daily Mail.
No comments