Korea Kaskazini: Tutakishambulia kisiwa cha Marekani siku chache zijazo

PYONGYANG-
SERIKALI inasema mpango wake ya kufyatua makombora kwenda kisiwa cha Marekani
cha Guam, utakuwa tayari hivi karibuni huku majibizano ya kivita na Marekani
yakiendelea.
Vyombo vya
habari nchini, vilieleza kuwa makombora ya Hwasong-12 yatapita anga ya Japan na
kuanguka baharini karibu kilomita 30 kutoka kisiwa cha Guam ikiwa mpango huo
utaidhinishwa na Rais Kim Jong-un.

Serikali imepuuza
onyo la Rais wa Marekani, Donald Trump kuwa itashambuliwa vikali. Marekani
imeionya Korea Kaskazini ikisema kuwa, vitendo vyake vinamaanisha kuwa huo
utakuwa mwisho wa utawala wa nchi hiyo.
Waziri wa Ulinzi
wa Marekani, Jim Mattis alisema Korea Kaskazini itashindwa vibaya ikiwa
itaingia vitani na Marekani na washirika wake.
Korea
Kaskazini ilitangaza jana kuwa inachora mipango ya kufanya mashambulizi ya
makombora katika kisiwa hicho kilicho na kambi za jeshi la Marekani na watu
163,000
Taarifa
iliyotolewa baadaye, ilisema jeshi litakamilisha mpango huo ifikapo kati kati
mwa mwezi huu na kupeleka kwa kiongozi wao Kim Jong-un kuidhinishwa.
BBC
BBC
No comments