Maporomoko ya ardhi yaua 40 DRC

KINSHASA- WATU zaidi ya
watu 40, wameuawa kwenye janga la maporomoko ya ardhi ambalo limetokea Kaskazini
Mashariki mwa nchi katika eneo la karibu na Ziwa Albert.
Wengi
wa wale waliopoteza maisha katika tukio hilo, ni watu wa kijiji kimoja
kinachofanya uvuvi katika kingo za Ziwa Albert.
Mvua
kubwa imesababisha sehemu za mlima ulio karibu kuporomoka na kufunika kijiji
hicho kwa mujibu wa shirika la habari la AFP. Watu wengine kadhaa, walifariki
wakitafuta dhahabu kwenye migodi ya zamani.
Kumekuwa
na majanga mabaya ya maporomoko ya ardhi, katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri
ya Demokrasia ya Congo miaka ya hivi karibuni.
Janga
hilo linatokea baada ya mafuriko mabaya yaliyotekea kwenye mji wa Freetown
nchini Sierra Leone, siku ya Jumatatu ambapo zaidi ya watu 300 waliuawa.
Ripoti
zinasema kuwa watu 28 walizikwa jana huku 12 wengine walizikwa leo.
BBC
No comments