Header Ads

Polisi watibua shambulio la pili Barcelona



https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/A9F9/production/_97431534_cambrilspoliceepa.jpg

BARCELONA- MAOFISA wa polisi nchini, wanasema kuwa wamewaua watu watano katika mji wa Cambrils ili kuzuia jaribio la pili la shambulio baada ya shambulio la jana mchana kuua watu 13 na kujeruhi wengine wengi.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na Polisi, washambuliaji walikuwa wamevalia vilipuzi.
Watu 13 walifariki huku makumi wakijeruhiwa, baada ya gari dogo kuingia katika eneo la watu mjini Barcelona eneo la Las Ramblas jana mchana.
Dereva wa gari hilo alitoroka na bado anaswaka. Waziri Mkuu, Mariano Rajoy alisema kuwa lilikuwa shambulio la kijihadi.
Mamlaka sasa zinahusisha shambulio hilo la Barcelona pamoja na lile la Camrils, huku mlipuko ukiripotiwa katika nyumba moja juzi Jumatano jioni katika mji wa Alcanar ambapo mtu mmoja alifariki.
Awali, Ofisa Mkuu wa Polisi, Josep Lluis Trapero alisema kuwa inaonekana wakazi wa eneo la Alcanar walikuwa wakiandaa kutengeneza kilipuzi.
Mjini Cambrils, watu saba akiwemo ofisa mmoja wa polisi walijeruhiwa wakati gari lilipovurumishwa katika umati wa watu mapema leo kulingana na huduma za dharura huko Catalan.
Mtu mmoja yuko katika hali ya mahututi.
Vyombo vya habari nchini, vimeripoti kwamba washambuliaji waliuawa wakati walipojaribu kutoroka baada ya gari lao kupinduka. Baadaye misururu ya milipuko ilifuatia.
BBC

No comments

Powered by Blogger.