Kombora la kivita lililoibwa lalipuka kiwandani Urusi

CHITA- Kombora
la kutungua ndege ambalo lilikuwa limebiwa na watu wasiojulikana, limelipuka na
kuwaua watu wawili na kumjeruhi mmoja nchini.
Kombora hilo
la urefu wa mita 10 (futi 35) ambalo liliundwa wakati wa enzi za Sovieti,
lililipuka likiwa katika kiwanda cha kutengeneza bidhaa mpya kutoka kwa bidhaa chakavu
Mashariki mwa nchi.
Vyombo vya
habari nchini, vilifahamishwa kuhusu mlipuko wa kombora hilo kubwa mjini hapa,
baada ya video ya mlipuko huo iliyokuwa imepigwa na mtu mmoja akitumia kamera
ya gari kuiweka YouTube.
Kombora hilo
ni la aina ya S-200 Angara, ambayo hufahamika kama SA-5 ‘Gammon’ katika mataifa
ya Nato.
Makombora
hayo yamekuwa yakitumiwa tangu miaka ya 1960, lakini siku hizi nafasi yake
imeanza kuchukuliwa na makombora aina ya S-300 na S-400. Haijabainika ni vipi
kombora hilo lilifika katika kiwanda hicho.
Tovuti ya
by24.org, inasema kwamba kombora hilo la uzani wa tani saba liliibiwa kutoka kwenye
kambi ya jeshi na watu wasiojulikana na kuuziwa wakuu wa kiwanda hicho.
Lililipuka wakati
wafanyakazi walipokuwa wakijaribu kulibomoa. Tovuti ya The Insider, ilisema
wafanyakazi wa dharura walipata kombora jingine aina ya S-200 ambalo halikuwa
limebomolewa.
Kisa hicho
kimezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii, wengi wakishangaa ilikuwaje
hadi kombora likawa katika kiwanda hicho.
“Tuna silaha
nyingi chakavu nchini, kiasi kwamba watu wanaziuza kama vyuma vikukuu,”
aliandika mmoja wa watu kwenye mtandao wa VKontakte. Alisema hilo linaweza
kusababisha madhara makubwa.
BBC
No comments