China kusitisha uagizaji wa malighafi kutoka Korea Kaskazini

BEIJING-
SERIKALI imesema leo kwamba, itasitisha uagizaji wa makaa yam awe, chuma cha
pua na bidhaa nyinginezo ambazo zimekuwa zikiiagizwa kutoka Korea Kaskazini
ndani wa wiki tatu zijazo ili kutekeleza vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa
Mataifa (UN).
China
ambao ndiyo washirika wakuu wa Korea Kaskazini, wamekuwa wagumu kutekeleza vikwazo
hivyo wakihofia utawala wa Kim Jong-un huenda ukaanguka lakini kwa sasa imeamua
na imezuia uagizaji huo kuanzia Agosti 5, mwaka huu.
Wakala
wa Forodha nchini, imesema itasitisha uingizwaji wa bidhaa kama vile makaa ya
mawe, chuma, samaki na chuma cha pua kufikia usiku wa Septemba 5, mwaka huu.
“Tunapenda
kutangaza rasmi kwamba, baada ya Septemba 5, mwaka huu, bidhaa hizo zitapigwa
marufuku kuingizwa nchini,” ilisema taarifa ya wakala wa forodha.
Tangazo
hilo linafuatia majibizano makali, baina ya Rais wa Marekani, Donald Trump na
kiongozi huyo wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un wiki iliyopita.
Korea
Kaskazini imekuwa ikiiuzia China bidhaa zenye thamani ya dola za Marekani
bilioni 1 (sh trilioni 2.2) kwa mwaka, hivyo hatua hiyo a China inatarajiwa
kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa taifa hilo lililopo rasi ya Korea.
VOA.
No comments