Header Ads

Kivumbi cha EPL chashuhudia nyavu zikitikishwa mara 31



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgWm_XBmoFf-bJeDr7U33c2Fv9G56b0RcVHysyU5K7k3gEoZ7C0-bJwG7ANd8U0Owo0Zn4RaY_46bf7aMEnfvY5zPsiticrjDr9cQfbhTc4Llg1eBtH3u3hx_faDYbRB5eqApUlwJJZeaKm/s1600/EPL+Stats+2016-17++Top+Scorers%252C+Most+Assist%252C+Clean+Sheets.jpg

LONDON- PAZIA la Ligi Kuu nchini (EPL), limefunguliwa rasmi Ijumaa ilyopita kwa mechi kali baina ya Arsenal na Leicester City na michezo mingine ambayo ilishuhudia nyavu zikitikiswa mara 31.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza na uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki wengi, ulishuhudia jumla ya mabao 7 yakitinga nyavuni mwa timu zote mbili.
Arsenal ndiyo waliokuwa wa kwanza kuandika bao lao kupitia kwa mshambuliaji wao mpya Alexandre Lacazette, mnamo dakika ya kwanza kabla ya kusawazishwa na Jamie Vardy.
Mara baada ya mabayo hayo, mchezo huo ulishuhudia bao tano nyingine zikitingisha nyavu. Arsenal wailazimika kusawazisha na kisha kuibuka na ushindi wa bao 4-3.
Michezo mingine ambayo ilifuata Jumamosi, ilikuwa ni baina ya Liverpool na Watford, mchezo ambao ulihusisha mabao sita baada ya kuisha kwa sare ya bao 3-3.
Chelsea ambao mabingwa hao watetezi waliangukia pua kwa kufungwa bao 3-2 na Burnley, huku wababe hao wa Stamford Bridge wakiwapoteza Garry Cahill na Cesc Fabregas ambao walioneshwa kadi nyekundu kila mmoja. Crystal Palace waliduwazwa na wageni Huddersfield Town kwa kuchapwa bao 3-0.
Bao pekee la Wayne Rooney, liliiwezesha klabu yake ya utotoni ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stoke City. Ingizo jipya la West Bromwich Albion, Ahmed Hegazy, liliing’arisha timu hiyo kwa kufunga bao lililoipa ushindi wa 1-0 dhidi ya AFC Bournemouth.
Mchezo wa jioni baina ya Manchester City dhidi ya wageni wa ligi, Brighton Hove and Albion, ulishuhudia City ikiibuka na ushindi wa bao 2-0 kwa magoli ya Sergio Aguero na Lewis Dunk aliyejifunga.
Jana Jumapili, EPL iliendelea kwa michezo miwili baina ya Newcastle United vs Tottenham Hotspurs na Manchester United na West Ham United.
Spurs iliibuka na ushindi wa bao 2-0, kupitia Dele Alli na Ben Davies huku Jonjo Shelvey akioneshwa kadi nyekundu, baada ya kumkanyaga makusudi Dele mbele ya mwamuzi.
Man United waliibuka na ushindi wa bao 4-0, kupitia kwa Romelu Lukaku aliyefunga mara mbili kabla ya Paul Pogba na Anthony Martial kufunga goli moja moja.
Vinara wa magoli hadi kufikia sasa ni;
Jina la Mchezaji
Timu anayotoka
Idadi ya magoli
Jamie Vardy
Leicester City
2
Steve Mounie   
Huddersfield Town)               
2
Romelu Lukaku   
Manchester United)             
2
Alexandre Lacazette
Arsenal
1
Shinji Okazaki
Leicester City
1
Aaron Ramsey                              
Arsenal     
1
Danny Welbeck
Arsenal
1
Olivier Giroud                               
Arsenal   
1
Stefano Okaka    
Watford     
1
Abdoulaye Doucoure                 
Watford  
1
Miguel Britos                                
Watford  
1
Sadio Mane                                  
Liverpool
1
Paul Pogba
Manchester United
1
Anthony Martial
Manchester United
1
Dele Alli
Tottenham Hotspurs
1
Ben Davies
Tottenham Hotspurs
1










No comments

Powered by Blogger.