CIA: Hakuna uwezekano wa kutokea vita vya nyuklia na Korea Kaskazini

WASHINGTON DC- MKURUGENZI wa Shirika la Ujasusi Marekani (CIA), Mike
Pompeo ameeleza kuwa hakuna uwezekano wala tishio lolote la kutokea vita vya nyuklia
baina ya Marekani na Korea Kaskazini licha ya kuongezeka kwa msukosuko.
Pompeo
alisema kuwa, Korea Kaskazini inaendelea kwa kasi na mipango yake ya nyuklia na
jaribio lolote la kombora halitakuwa la kutia wasiwasi.
Hata hivyo,
Pompeo ameonya kuwa uvumilivu wa Marekani unafikia kikomo. Pande zote mbili
zimetupiana maneno makali huku Rais Donald Trump akitishia kuikabili vikali
Korea Kaskazini.
Pompeo anasema
ana uhakika kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un atajaribu kuendelea
na mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.
Alipoulizwa
kuhusu muda gani Korea Kaskazini wamebaki nao, kabla ya kuunda silaha ya nyuklia
ambayo inaweza kushambulia Marekani, alisema kuwa wako karibu.
Msukosuko wa
siku nyingi kuhusu mpango wa nyukilia wa Korea Kaskazini, uliongezeka zaidi
wakati taifa hilo lilipofanya jaribio la makomboa mawili ya masafa marefu mwezi
uliopita.
Hatua hiyo,
ilisababisha awamu nyingine ya vikwazo vya kiuchumi vya Umoja wa Mataifa hatua
iliyoghadhabisha utawala wa Kim.
Trump
alisema kuwa jeshi la la Marekani liko tayari, huku Korea Kaskazini ikimlaumu
kwa kuchochea vita katika rasi ya Korea.
BBC
No comments