Header Ads

Kiongozi wa upinzani Zambia aachiwa huru



https://ichef-1.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/17534/production/_97404559_a1031ff1-f7d1-4c02-b5e6-93b8e1d5b7d5.jpg

LUSAKA- KIONGOZI wa upinzani nchini, Hakainde Hichilema ambaye anakabiliwa na mashataka ya uhaini ameachiliwa huru, kwa mujibu wa chama chake.
Hichilema alikamatwa Aprili mwaka huu, baada kudaiwa kuhatarisha maisha ya Rais Edgar Lungu kwa kukataa kuupisha msafara wa Rais Edgar Lungu wakati viongozi hao wakielekea kwenye sherehe za kitamaduni Magharibi mwa nchi.
Kiongozi huyo wa chama cha UPND pamoja na wafuasi wake watano, walifunguliwa mashtaka ya uhaini, ambayo ni makosa yasiyokuwa na dhamana kwa kulingana na sheria za Zambia. Walikana mashtaka hayo.
Taarifa zilieleza mapema kuwa kuachiliwa kwake ni sehemu ya makubaliano yaliyoongozwa na Jumuiya ya Madola.
Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Patricia Scotland, alikuwa nchini wiki iliyopita ambapo alikutana na Rais Lungu na Hichilema. Baadaye alisema kuwa, Hichilema ataachiliwa kwa manufaa ya nchi.
BBC

No comments

Powered by Blogger.