Raila kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani

NAIROBI- KIONGOZI wa Muungano
wa Upinzani na aliyekuwa mgombea wa urais Kenya, Raila Odinga amesema atakwenda
Mahakama ya Katiba kwa ajili ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Agosti
8, mwaka huu.
Akizungumza na
waandishi wa habari na wananchi waliojitokeza kumsikiliza, Raila alisema
maamuzi hayo yamefikiwa kutokana na NASA kutoridhishwa na mwenendo mzima wa
uchaguzi huo na kuongeza kuwa matokeo yalichakachuliwa.
Aidha, Raila alisema
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC) ilitangaza matokeo hayo huku
kukiwa na upungufu wa baadhi ya fomu za kujumlishia matokeo maarufu kama 34A na
34B.
“Kama NASA,
hatujaridhishwa na namna mchakato wa kuhesabu na kutangaza matokeo uluvyokuwa.
Hivyo tunakwenda Mahakama ya Katiba kupinga matokeo yaliyotengenezwa kwa
kompyuta, ili kumpa ushindi Uhuru Kenyatta na mwenzake William Ruto,”
“Wakenya wanahuzunika
kwani walijitokeza kwa wingi, ili kuchagua kiongozi wanayempenda lakini sauti
yao imemezwa na kompyuta iliyotumika kuzalisha matokeo hayo na kuipa ushindi
Jubilee,” alisema Raila.
No comments