Ronaldo ashushiwa rungu kali Hispania
MADRID-
MSHAMBULIAJI mahiri wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (32) amefungiwa kucheza
mechi tano baada ya kumsukuma mwamuzi aliyemuonesha kadi nyekundu kwenye mchezo
dhidi ya mahasimu wao wakubwa Barcelona jana.
Mreno
huyo ambaye aliingia akitokea benchi, aliifungia timu yake bao la pili ambalo
lilisababisha apewe kadi ya njano kwa kuvua jezi. Kadi ya pili ya njano na
nyekundu, zilikuja baada ya mchezaji huyo kudaiwa kujiangusha kwa ajili ya
kutafuta penati.
Mara
baada ya kujiangusha, mwamuzi wa mchezo huo alimuonesha Ronaldo kadi ya pili ya
njano kisha nyekundu ambayo ilisababisha mchezaji huyo kumsukuma mwamuzi huyo.
Kwa
mujibu wa taarifa ya shirikisho la soka Hispania, Ronaldo anakosa mchezo mmoja
kutokana na kadi hizo na mingine minne ikiwa ni adhabu ya kitendo cha utovu wa
nidhamu cha kumsukuma mwamuzi.
Ronaldo
atakosa mchezo wa marudiano dhidi ya Barcelona kwenye kombe hilo la Super Cup,
unaotarajiwa kuchezwa Jumatano jijini hapa. Pia mchezaji huyo atakosa michezo
mingine minne ya La Liga dhidi ya Deportivo La Coruna, Valencia, Levante na
Real Sociedad.
Hata
hivyo, Real Madrid wamepewa siku 10 za kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Independent.
No comments