Header Ads

China yafungua kambi ya kijeshi Djibouti



China hatimaye imefungua rasmi kambi yake ya kijeshi katika taifa la Djibout siku ya Jumanne kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

DJIBOUTI CITY- HATIMAYE China imefungua rasmi kambi yake ya kijeshi nchini, ambayo ni ya kwanza kufunguliwa na Jeshi la Maji la taifa hilo.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters, kambi hiyo iliyofunguliwa leo, inaonesha kutimia kwa azma ya taifa hilo ambalo ilianza ujenzi wa kituo hicho cha mipango nchini hapa mwaka uliopita.
Kambi hiyo, itatumika kusambaza meli za wanamaji wake wanaoshiriki shughuli za kulinda amani na mipango ya kibinadamu katika pwani ya Yemen na hususan Somalia.
Ni kambi ya kwanza ya wanamaji katika taifa la kigeni, ijapokuwa maofisa wa China wameitaja kuwa eneo la kupanga mikakati. Kambi hiyo itasaidia China kuimarisha doria zake katika maji yasiyo ya Somalia na Yemen, mbali na kutekeleza majukumu yake ya kibinadamu.
Licha ya Djibout kuwa na eneo dogo, ina kambi za kijeshi za Marekani na Ufaransa.

No comments

Powered by Blogger.