Breaking News; Serge Aurier kusaini miaka 5 Man United

PARIS- BEKI wa pembeni wa PSG na Ivory
Coast, Serge Aurier (24) ameripotiwa kukubali kusaini mkataba wa miaka mitano
na Manchester United ya Uingereza.
Hata hivyo, makubaliano hayo yanaelezwa
kuwa bado kwani Manchester United na PSG hawajaafikiana kuhusu ada kamili ya
mchezaji huyo ambaye amekuwa akiwindwa na mabingwa wa EPL, Chelsea.
Kwa sasa timu hizo ziko katika
mazungumzo kuhusu ada ya uhamisho ambayo inadaiwa kuwa ni karibu na pauni
milioni 30 (sh bilioni 87).
The Sun.
No comments