Asubuhi Yetu; Liverpool yamsaka mbadala wa Coutinho # Costa aigomea Chelsea # Tottenham wamfuata Serge Aurier

LIVERPOOL- KLABU ya Liverpool imeingia katika mbio za
kusajili wachezaji wawili, Renato Sanches (19) kutoka Bayern Munich, ilia je azibe
pengo la Philippe Coutinho akiondoka klabuni hapo. Pia wanamtaka winga wa
Monaco, Thomas Lemar (21). Le10Sport.

Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa (28) hataripoti klabuni hap oleo,
wakati wachezaji wenzake wote watakaporipoti kwa ajili ya maandalizi ya msimu
mpya, kutokana na mchezaji huyo kushinikiza kuondoka Stamford Bridge. Daily
Mirror.

Tottenham na Inter Milan wameingia kwenye vita ya kuwania kumsajili beki
wa PSG, Serge Aurier (24) wakiwa na matumaini kuwa bei ya mchezaji huyo
itapungua. ESPN.

Beki wa kati wa Southampton, Virgil van Dijk (26) anatarajiwa kukutana na
kocha wa timu hiyo, Mauricio Pellegrino kwa ajili ya mazungumzo kuhusu
uhamisho. Liverpool watakuwa wakifuatilia kwa karibu mazungumzo hayo ambayo
yataamua hatima ya Virgil. Liverpool Echo.
Kinda wa Manchester City, Jadon Sancho (17) anaweza akaondolewa klabuni
hapo, baada ya kushindwa kutokea mazoezini kwa mara kadhaa bila taarifa maalum.
Telegraph.

Inter Milan wanajiandaa kuipiku Arsenal, kwenye usajili wa beki wa timu
ya Nice ya Ufaransa, Dalbert (23) kwa ada ya pauni milioni 17 (sh bilioni 49.3).
Talksport.
Newcastle United wamesema wanahitaji kumsajili mshambuliaji wa Arsena,
Lucas Perez (28) lakini hawawezi kufikia bei ya pauni milioni 13.4 (sh bilioni 38.8)
inayotakiwa na washika bunduki hao wa London. London Evening Standard.

Everton wanajiandaa kutoa dau lao la mwisho la pauni milioni 50 (sh
bilioni 145) na beki wao, Callum Connolly (19), kwa ajili ya kumsajili kiungo
mshambuliaji wa Swansea City, Gylfi Sigurdsson. Wales Online.
Timu mbalimbali za Ligi Kuu ya Italia, Cagliari, Sassuolo na Verona
zimeonesha nia ya kumsajili beki wa Arsenal, Carl Jenkinson (25). Corriere
dello Sport.
No comments