Header Ads

Mwizi akutwa amelewa chakari ndani ya nyumba aliyovunja



Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa polisi nchini Australia baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani.

ESPERANCE- MTU mmoja amefunguliwa mashtaka na maafisa wa polisi nchini, baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja na kisha kunywa shampeni na kulala kitandani.
Polisi wanadai mwanaume huyo mwenye miaka 36, alivunja na kuingia katika nyumba hiyo mjini hapa, Ijumaa ya wiki iliyopita.
Inadaiwa kuwa, mtuhumiwa huyo alilewa baada ya kunywa kinywaji hicho. Mwenye nyumba alirudi nyumbani na kumkuta mwizi huyo amelala kitandani mwake.
“Alitoka nje na kuwapigia simu polisi, ambao walifika na kumkamata mtuhumiwa,” alisema Sajenti Richard Moore.
Moore alisema polisi walilazimika kumpeleka mtuhumiwa huyo hospitalini, baada ya kukutwa amelewa chakari na atafunguliwa mashtaka ya wizi.
BBC.

No comments

Powered by Blogger.