Header Ads

Asubuhi Leo; Chelsea wamtaka Belotti # Arsenal kukataa ofa za Sanchez # Juventus wamtaka Fellaini



http://i1.mirror.co.uk/incoming/article9588598.ece/ALTERNATES/s615/Andrea-Belotti-of-Torino-FC-celebrates-after-scoring-the.jpg

LONDON- CHELSEA wanadaiwa kuanza kumuwinda mshambuliaji wa Torino ya Italia, Andrea Belotti lakini bado haijawekwa wazi wameweka dau lenye thamani gani. Belotti anatakiwa ili azibe pengo la Diego Costa. Daily Star.

http://cdn.images.dailystar.co.uk/dynamic/58/photos/949000/620x/Alexis-Sanchez-637200.jpg
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema klab hiyo itakataa ofa yoyote itakayoletwa na timu yoyote kama ada za uhamisho za Alexis Sanchez na Alex Oxlade-Chamberlain. Wenger anatarajia wachezaji hao wataheshimu mikataba yao. Daily Mirror.

http://img.bleacherreport.net/img/images/photos/003/563/909/hi-res-e914f8b710e5b9a0d0d3b7b317ab6c2b_crop_north.jpg?h=533&w=800&q=70&crop_x=center&crop_y=top
Liverpool imeiambia Barcelona kwamba, ofa yoyote kutoka kwa wababe hao wa Hispania yenye nia ya kumnunua Philippe Coutinho ni lazima ihusishe uwepo wa kiungo Ivan Rakitic.  Daily Express.

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2016/01/13/09/3019584F00000578-3397162-image-a-26_1452678972921.jpg
Klabu ya Juventus ya Italia, imemuorodhesha kiungo wa Manchester United, Marouane Fellaini kama mchezaji namba moja kati ya wengi wanaotakiwa na mabingwa hao wa Serie A. Sun.

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2017/06/20/11/4192BB9A00000578-0-image-a-64_1497954802293.jpg
Jaribio la Chelsea kutaka kumsajili beki wa Juventus, Alex Sandro, limegonga mwamba baada ya wababe hao wa Ligi Kuu ya Italia kukataa ofa iliyowasilishwa na mabingwa wenzao kutoka Uingereza. Daily Mail.

http://cdn.images.express.co.uk/img/dynamic/67/590x/Geoffrey-Kondogbia-718420.jpg 
Kiungo Mfaransa anayekipiga Inter Milan, Geoffrey Kondogbia, ameambiwa afanye mazoezi peke yake kufuatia kukwaruzana na uongozi wake. Kondogbia anawindwa na Liverpool na Tottenham. Talksport.

https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/08/nintchdbpict0003404198645.jpg?strip=all&w=960&quality=100
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amemtaka Diego Costa awasilishe barua ya kuomba kuuzwa klabuni hapo. Tayari timu hiyo inadaiwa kuzipiga chini ofa mbili zenye thamani ya pauni milioni 52 (sh bilioni 150.8) na pauni milioni 61 (sh bilioni 176.9). London Evening Standard.

http://i2.cdn.cnn.com/cnnnext/dam/assets/160215110254-serge-aurier-exlarge-169.jpg
Tottenham wanadaiwa kufikia makubaliano na beki wa PSG, Serge Aurier. Awali mchezaji huyo alidaiwa kukubaliana maslahi binafsi na Man United, lakini kibali cha kuingia Uingereza kilizua utata. L’Equipe.

http://breakingthelines.com/wp-content/uploads/2017/05/cedric-soares.jpg
Chelsea imehamishia akili zao, kwenye mpango wa kumsajili beki wa Southampto, Cedric Soares, wakati timu hiyo ikijaribu kusajili wachezaji kadhaa ili kuimarisha kikosi chao kwenye dirisha hili kubwa. Telegraph.

http://i2.mirror.co.uk/incoming/article9751445.ece/ALTERNATES/s1200/William-Carvalho.jpg
Mazungumzo baina ya West Ham na Sporting Lisbon yamekwama, kutokana na timu hizo kutoafikiana kuhusu ada ya usajili wa William Carvalho. Sporting wanataka pauni milioni 40 (sh bilioni 116). Sun.



No comments

Powered by Blogger.