Asubuhi Leo; Barcelona wakwama Dortmund # Real Madrid wateta na Dybala # Chelsea wamfuata Cancelo

DORTMUND- BARCELONA wamewasilisha mezani ofa yenye
thamani ya pauni milioni 90 (sh bilioni 261), kwa Borussia Dortmund ili
kumsajili kinda wa Ufaransa, Ousmane Dembele (20) anayekipiga Signal Iduna
Park. Hata hivyo dau hilo limekataliwa. Sky Sports.
PSG wanakaribia
kumsaini kinda hatari wa Monaco, Kylian Mbappe (18) kwa dau linalodaiwa kuwa pauni
milioni 180 (sh bilioni 522). Mchezaji huyo amekuwa akiwindwa na Real Madrid,
Manchester City na Arsenal. Gazzetta dello Sport.
Real Madrid inadaiwa kukutana kwa siri na kufanya
mazungumzo na windo la Barcelona, Paulo Dybala (23) kwa ajili ya kuangalia
uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo wa Juventus na Argentina. Don Balon.
Chelsea wameendelea kutumaini kuwa Valencia
watawakubalia ofa yao ya kumsajili beki wao, Joao Cancelo (23). Sky Sports.
Kocha wa
Manchester United, Jose Mourinho ameliweka jina la Danny Rose (27) nafasi ya
kwanza katika orodha ya majina ya wachezaji anaowahitaji kwa ajili ya msimu
ujao. Daily
Record.

Arsene
Wenger amesema klabu yake ya Arsenal haina matumaini makubwa ya kumshawishi
staa wa timu hiyo, Alexis Sanchez (28) kubaki Emirates. Pia timu hiyo imempa ofa
ya mshahara wa pauni 300,000 (sh milioni 870) kwa wiki. Daily Mail.
Mchambuzi wa soka la Hispania, Graham Hunter amesema
Barcelona hawataweza tena kumsajili kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho
(25), iwapo watafanikiwa kumsainisha winga wa Borussia Dortmund, Ousmane
Dembele (20). BBC Radio 5.
Mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs, Daniel Levy yuko
katika mtanziko mkubwa kuhusu mishahara kiduchu wanayolipwa wachezaji wa timu
hiyo. Wengi wametishia kuondoka wakiongozwa na Danny Rose (27) ambaye Levy
amesema atamuuza kwa pauni milioni 50 (sh bilioni 145). Daily Mail.

Arsenal wana matumaini ya kumbakiza klabuni hapo
kiungo wao, Mesut Ozil (28), baada ya Mjerumani huyo kusema anajiandaa kukubali
mshahara wa pauni 225,000 (sh milioni 652.5) kwa wiki. The Sun.

PSG wanajiandaa kumtoa mshambuliaji wao Javier
Pastore (28) na fedha, kwa ajili ya kumsajili kipa wa Atletico Madrid na Slovenia,
Jan Oblak (24). AS.
West Ham wameweka mezani mwa Sporting Lisbon dau la
pauni milioni 30 (sh bilioni 87), kwa ajili ya kupata huduma ya kiungo wa timu
hiyo ya Ureno, William Carvalho (25). Telegraph.
No comments