WHO yaonya kisonono kimeanza kuwa sugu
GENEVA- SHIRIKA
la Afya Duniani (WHO), limetoa tahadhari kuwa, ugonjwa wa zinaa wa kisonono (Gonorrhoea)
umeanza kuwa sugu dhidi ya dawa ya kupambana nao.
Kwa mujibu
wa utafiti uliofanywa katika mataifa 77 tofauti Duniani, imebainika kuwa
maambukizi ya ugonjwa huo katika mataifa ya Japan, Ufaransa na Hispania,
hayatibiki kabisa.
Hata hivyo,
shirika hilo linasema wengi wanaoambukizwa ugonjwa huo wako katika nchi
masikini, ambazo zina vifaa duni kudhibiti ugonjwa huo.
WHO linasema kufanya mapenzi bila ya kinga na kuwa
na wapenzi wengi, kunachochea kuenea kwa ugonjwa huo.
BBC
No comments