Melivita ya China yafanya ziara Hong Kong
BEIJING- MELIVITA
ya kwanza ya China iitwayo Liaoning, yenye uwezo wa kubeba ndegevita imewasili
mjini Hong Kong.
Ziara hiyo
ya kwanza nje ya China bara, ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 20 tangu
Uingereza ilipoikabidhi Hong Kong kwa China.
Hayo yanajiri
muda mfupi baada ya ziara ya Rais Xi Jinping katika mji huo wiki iliyopita,
ikiwa ni ya kwanza kama Rais wa China. Wakati wa ziara yake, ambayo ilikabiliwa
na maandamano, alionya kwamba changomoto yoyote kwa serikali ya beijing
haitakubalika.
Haki ya
kisiasa ya Hong Kong imezua wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni, huku kukiwa
na mwito wa kujitawala pamoja na kupigania uhuru.
Mwaka 2014, China
ilisema kuwa itaruhusu uchaguzi wa moja kwa moja wa kiongozi wa mji huo, lakini
miongoni mwao wawepo wagombea waliokubalika na China.
Hatua hiyo
ilisababisha maandamano yaliojulikana kuwa mwavuli, yakitaka uhuru katika
uchaguzi huo. Ziara hiyo ya Xi ilijiri huku kukiwa na usalama mkali.
Baada ya Rais
Xi kuondoka Jumamosi iliyopita, maelfu ya wananchi waliandamana wakitaka haki
yao ya kidemokrasia.
No comments