Mvua kubwa yaua sita Japan
KYUSHU- WATU
sita wamekufa na wengine 100,000 wametakiwa kuondoka katika makazi yao kisiwani
hapa, baada ya mvua kubwa zinazonyesha kusababisha mafuriko makubwa zaidi.
Mvua ambazo
zilinyesha kwa saa 40 mfululizo katika baadhi ya sehemu, zilisababisha mafuriko
kwani ni kubwa zaidi ya zile ambazo zimekuwa zikinyesha kawaida miezi hii.
Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, lililazimika kutumia helikopta kuokoa mamia ya watu
waliokwama kwenye paa za nyumba zao na kwenye miti kutokana na mafuriko hayo.
Mbali na
kuwepo kwa jeshi hilo la zimamoto, vikosi vingine vya majeshi vililazimika kuja
kuongeza nguvu kwenye zoezi hilo la uokoaji na kufanikiwa kuwaokoa watu wengi.
Sky News
No comments