Waziri Mkuu Pakistan ajiuzulu
ISLAMABAD- WAZIRI
Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif amejiuzulu wadhifa huo baada ya Mahakama Kuu
nchini kumzuia kushika wadhifa wowote Serikalini kufuatia uchunguzi kwa madai
ya ufisadi.
Uamuzi huo,
unakuja baada ya uchunguzi kuhusu utajiri wa familia yake na ufichuzi wa mwaka
2015 wa Panama Papers, uliowahusisha watoto wake na akaunti za benki ugenini.
Sharif mara
kwa mara amekuwa akikana kufanya lolote baya.
Amri hiyo
ilitolewa na jopo la majaji watano. Mahakama ilifurika leo na usalama zaidi uliimarishwa
katika viunga vyote vya mahakama hiyo na mji huu huku maelfu ya wanajeshi na
polisi wakimwagwa mitaani.
Waziri wa Mambo
ya Ndani nchini nchini, Chaudhry Nisar Ali Khan, alimshauri Sharif kukubali
uamuzi wa leo.
Mahakama
imependekeza kufunguliwa kwa kesi za ufisadi, dhidi ya watu kadhaa akiwemo Sharif,
mtoto wake wa kike, Maryam na mumewe Safdar, Waziri wa Fedha, Ishaq Dar na
wengine kadhaa.
Hakuna Waziri
Mkuu wa Pakistan aliye raia ambaye alishawahi kumaliza kipindi chake cha miaka
mitano cha uongozi.
No comments