Mahakama ya Rufaa yatupilia mbali rufaa kupinga ushindi wa Bulaya
DAR ES SALAAM- Mahakama ya Rufaa nchini,
imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na wapiga kura 4 wa
Jimbo la Bunda Mjini kupinga ushindi wa Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chadema, Esther Bulaya.
Rufaa hiyo iliwasilishwa mahakamani
hapo na wapiga kura hao, ambao walikuwa wakidai Bulaya alishinda visvyo halali.
Mara baada ya uamuzi huo ambao ulimpa
ushindi mbunge huyo, Bulaya kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika: “Wana
Bunda wameshinda tena na tena,asante Mungu.”
No comments