Aliyeua wazazi na majirani 17 ahukumiwa kifo China
YUNNAN- MWANAUME
mmoja ambaye aliwaua wazazi wake, kisha kuwaua majirani 17 ili kuficha siri
amehukumiwa kifo na mahakama ya jimbo.
Yang Quingpei
ambaye aliwaua wazazi wake wote wawili, baada ya wazazi kukataa kumkopesha
fedha za kwenda kulipa madeni aliyokuwa nayo.
Mara baada
ya kutekeleza mauaji hayo ya wazazi wake, inadaiwa kuwa Yang alipata wasiwasi
kuwa huenda majirani wamemuona na ndipo alipoua watu wa familia sita za jirani
wakiwemo watoto watatu kwa kutumia sururu ndogo.
Inadaiwa kuwa
Yang alitoroka, lakini alikamatwa katika mji wa Kunming siku moja baada ya
tukio. Kwa mujibu wa Shirika la Habari
la China, katika hukumu yake mahakama ya jimbo ilieleza tukio hilo kuwa la
kinyama, kikatili na la kutisha.
“Japokuwa
amekiri mwenyewe kutekeleza ukatili huo, na kuelezea masikitiko yake baada ya
kuletwa mbele ya sheria, hayo hayatoshi kusababisha ahurumiwe kwenye hukumu
yake,” ilisema sehemu ya hukumu.
Sky News
No comments