Waziri adaiwa kutumia bilioni 1.6/- kununua maua na zawadi Afrika Kusini
DURBAN-
CHAMA kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance (DA), kimesema kitaomba
maelezo ya kina kuhusiana na mayumizi ya fedha zenye thamani ya dola za
Marekani 770,000 (sh bilioni 1.6).
Fedha hizo
zinadaiwa kutumiwa visivyo mwaka wa fedha 2013/14 na Wizara ya Nyumba na Makazi
iliyo chini ya Waziri Lindiwe Sisulu, ambaye ni mtoto wa mpigania uhuru wa
Afrika Kusini, Walter Sisulu.
Inadaiwa kuwa,
fedha hizo ambazo zinaweza kujenga nyumba 100 za bei nafuu, zilitumika kununua
maua na zawadi mbalimbali kwa watumishi wa idara hiyo.
Kubainika kwa
matumizi ya fedha hizo, kumekuja hivi karibuni wakati waziri huyo akijibu moja
ya maswali yaliyoelekezwa kwake bungeni na kuzua mjadala mkubwa.
DA wanadai
kwamba, waziri huyo ambaye kwa sasa anapigania kuchaguliwa kuwania kupitishwa
na chama cha ANC kwa ajili ya kugombea urais, anapaswa kuwajibishwa ili ataje
wale wote walionufaika na mgawo wa fedha hizo.
BBC
No comments