Nyani akata umeme Zambia
LUSAKA- SHIRIKA
la Umeme Zambia (ZESCO), limeeleza kuwa tatizo la umeme kukatika jana katika
mji wa Livingstone lilitokana na hitilafu iliyosababishwa na mnyama aina ya
nyani.
Msemaji wa
Zesco, Henry Kapata, alieleza kuwa nyani huyo aliingia kwenye eneo lenye mitambo
mikubwa ya kupoza na kusambaza umeme na kisha kupigwa shoti iliyosababisha
kukatika kwa umeme kwa saa sita.
“Baada ya
nyani huyo kufanikiwa kupenya na kuingia kwenye mitambo hiyo, alipigwa na shoti
hiyo lakini cha ajabu ni kuwa hakufa. Alifanikiwa kupona lakini alikutwa na
majeraha mengi, na kisha kukabidhiwa kwa idara ya wanyama pori,” alisema
Kapata.
Aidha,
Kapata alisema kuwa tatizo hilo limefanikiwa kutatuliwa na umeme sasa umerudi
kwenye majimbo yote ya Kusini na Magharibi ambayo yalikumbwa na tatizo hilo.
“Angelikuwa
ni binadamu ndiye aliyesababisha tatizo hilo na hakufa, basi angekabiliwa na
kifungo cha miaka 10 hadi 25 jela,” alisema Kapata.
BBC
No comments