Header Ads

Lita nne za petrol zawaponza wanafunzi Kenya



http://www.capitalfm.co.ke/news/files/2017/07/KANGUNDO-LAW-COURTS.jpg

MACHAKOS- WANAFUNZI nane wa shule ya sekondari ya wavulana ya Kisukioni mjini hapa, wamefikishwa mahakamani leo wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama za kuchoma shule.
Akizungumza na Capital FM, Ofisa wa Polisi, James Njiiri, alieleza kuwa wanafunzi hao walikamatwa na kufikishwa katika mahakama ya Kangundo kwa kukutwa na lita nne za petrol.
Njiiri alieleza kuwa wanafunzi sita kati ya nane, wapo kidato cha tatu wakati wengine wawili wanasoma kidato cha nne na kuonya kuwa matukio kama hayo yanahatarisha maisha ya wanafunzi wenzao.
“Hatutavumilia tabia kama hizo wala hatutapindisha sheria kwa ajili ya kesi kama hizi kwenye shule zetu. Yeyote atakayekamatwa, atafikishwa mahakamani na sheria itachukua mkondo wake,” alisema Njiiri.
Hata hivyo, wanafunzi hao walikana mashtaka yao na kuachiwa kwa dhamana, baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya thamani ya sh 50,000 za Kenya (sh milioni 1 za Tanzania).
Capital News

No comments

Powered by Blogger.