Wapalestina wapinga hatua mpya za Israel

JERUSALEM- KIONGOZI
wa Palestina, Mahmoud Abbas anasema kuwa ataendelea kukata mawasiliano na
Israeli licha ya kuondolewa kwa mitambo ya kutambua chuma katika eneo Takatifu Mashariki
mwa Jerusalem.
Kuwekwa kwa
mitambo hiyo, kulisabaisha ghasia mbaya na Wapalestina ambao waliiona kama
hatua ya Israel kutaka kudhidti eneo hilo. Israel ilisema kuwa, ilikuwa muhimu
kuzuia silaha kuingizwa eneo hilo. Inasema sasa ina mipango ya kuweka kamara za
ulinzi.
Pande zote
ziko chini ya shinikizo kutoka jamii ya kimataifa kutatua mzozo huo, katika
eneo hilo takatifu ambalo kwa waislamu linajulikana kama Haram al-Sharif na kwa
wayahudi kama Temple Mount.
Mjumbe wa
Umoja wa Mataifa eneo la Mashariki ya Kati, ametaka misukosuko kupungua kabla
ya maombi ya Ijumaa ambayo huhudhuriwa na maefu ya watu. Hatua mpya za usalama,
zilichukuliwa kufuatia kuuliwa kwa polisi wawili wa Israel.
Licha ya
kuongezeka kwa misukusuko, ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, ilisema jana kuwa
itaondoa mitambo ya kutambua chuma na kuweka teknolojia tofauti iliyo bora.
Hatua mpya
zitawekwa ndani ya kipindi cha miezi sita inayokuja, huku polisi zaidi
wakiwekwa hadi wakati huo. Kulingana na shirika la habari la Reuters, watu
walionekana wakiondoa mitambo hiyo na kamera zilizowekwa juzi.
Lakini Rais Abbas
na kiongozi wa Kiislamu ambaye anasimamia eneo hilo takatifu, walitupilia mbali
mabadiliko hao wakitaka hali kurejea kawaida.
BBC.
No comments