Asubuhi Leo; Man City kutoa £160m kwa Mbappe # Lemar kutua Arsenal # Barcelona wamfuata Coutinho Uingereza
MANCHESTER- MANCHESTER City wanajipanga kuwapiku Real
Madrid, katika mchakato wa kumsajili mshambuliaji kinda wa Monaco, Kylian
Mbappe (18) kwa kutoa dau la kufuru la pauni milioni 160 (sh bilioni 464). Hata
hivyo, inadaiwa Mbappe huenda akakataa kutua City kwani anataitaka Madrid. Daily
Mirror.
Hatimaye Arsenal wanatarajiwa kukamilisha muda wowote, usajili wa winga
wa Monaco, Thomas Lemar (21), kwa ada ya pauni milioni 45 (sh bilioni 130.5). Sun.
Barcelona imetuma maofisa wake kuja nchini, ili kujaribu kumshawishi
mchezaji wa Liverpool, Philippe Coutinho (25), licha ya dau lao la pauni
milioni 72 (sh bilioni 208.8) kukataliwa na majogoo hao wa Anfield. Barca
wanatarajiwa kutoa pauni milioni 80 (sh bilioni 232). Daily Express.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema klabu hiyo haiogopi kufungua
pochi ili kusajili wachezaji wakubwa, wakati klabu hiyo ikiwa mbioni
kukamilisha usajili wa beki wa Southampton, Virgil van Dijk (26). Daily
Mirror.
Kiungo wa Bayern Munich na Ureno, Renato Sanches (19) amebainisha kuwa
ataondoka klabuni hapo msimu huu na kuongeza joto kwa klabu za Manchester
United na AC Milan ambazo zinamhitaji. Bayern wanataka pauni milioni 43 (sh
bilioni 124.7). Independent.
Tottenham Hotspurs wamejielekeza kwa beki wa Hoffenheim, Jeremy Toljan
(22) baada ya mazungumzo ya kumsajili beki wa Porto, Ricardo Pereira (23)
kukwama. Daily Mail.
Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere (25) amesema hataki kutoka nje ya
London, endapo ataamua kuondoka Arsenal. Inadaiwa kuwa anataka kuhamia West Ham
ambao wamekuwa wakimtaka. Independent.
Arsenal wanatarajiwa kupata hasara kubwa, kutokana na mshambuliaji wao,
Lucas Perez (28) kutaka kuondoka. Deportivo La Coruna ndiyo klabu pekee inayomtaka
na imetoa ofay a pauni milioni 9 (sh bilioni 26.1). Evening Standard.
No comments