Aliyefanya shambulizi kwa msumeno akamatwa Uswisi

GENEVA- POLISI
nchini, wamasema wamemkamata mtu mmoja aliyetambuliwa kama, Franz Wrouisis
ambaye anaaminika kufanya shambulizi la kuwajeruhi watu kwa kutumia msumeno mwanzoni
mwa wiki.
Shambulizi
hilo lilifanywa ndani ya ofisi moja ya umma Jumatatu ya wiki hii katika mji wa
Schaffhausen. Baada ya tukio hilo, Wrousis mwenye miaka 51 alimakatwa kilomita
60 nje ya mji huo ambako alitekeleza shambulizi hilo.
Wafanyakazi
watano kwenye ofisi hiyo inayohusika na masuala ya bima ya afya, walijeruhiwa
vibaya huku mmoja hali yake ikisemekana kuwa ni mbaya zaidi.
Mshukiwa
huyo alikuwa akifuatiliwa na polisi kabla ya tukio hilo.
BBC.
No comments